Google AdSense

Breaking News

Magoli yote ya Singida United vs Mwadui FC VPL


Haikua rahisi uwanja wa Namlia kw Singida united kutoka kwa ushindi wa magoli matatu kwa mawili dhidi ya Mwadui FC kwani dakika ya 10 tu mwanzo wa mchezo Mwadui waliandika goli la kwanza wakati Singida united wakihangaika kutafuta goli la kusawazisha Mwadui FC walifanikiwa kupata goli la pili mnamo dakika ya 30 kupitia kwa kiungo mshambuliaji Uwesu na jitihada za kutafuta kwa Singida united hazikufa mpaka mnamo dakika ya 32 wakafanikiwa kupata goli kupitia kwa Chuku na dakika ya 42 wakapata goli safi kabisa la kichwa kupitia kwa Kaseke akimalizia cross ya Mudathir Yahya na mpaka mapumziko timu hizo mbili zikaenda zikiwa na nguvu sawa (2-2)

Kipindi cha pili Singida united walikuja kwa kasi kutafuta goli la tatu lakini ilikuwa sio rahisi kupata goli hilo mapema kwani Mwadui FC walikuwa wakishambulia lango la Singida united kwa kushtukiza Lakini wanasema kama ipo ipo tu dakika 90 za kucheza zilimalizika na mwamuzi kuongeza dakika 5 ambazo zilionekana kuwa na faida kwa Singida united kuandika goli la ushindi mnamo dakika ya 93 kupitia kwa Keny Ally Mwambungu na kufanya matokeo kuwa (3-2) na Singida united kufikisha jumla ya pointi 30 

No comments