Alichokisema Samata kuelekea mchezo wa Taifa stars dhidi ya Congo
Timu ya taifa ya Tanzania Taifa stars waahidi kufanya vizuri kwenye mchezo wao wa kirafiki dhidi ya Congo DRC hapo kesho 27 Mach 18 , Wamesema wachezaji hao wakiongozwa na nahodha wao Mbwana Samata anaekipiga huko Ubelgiji kwenye klabu ya Genk akiwa na rekodi ya kuifanyia vizuri timu yake kwani amekua akiisaidia timu yake kupata matokeo licha ya ushindani ambao upo kwenye klabu kuwa na wachezaji wengi nyota.
Ikumbukwe mechi ya mwisho Taifa stars walicheza dhidi ya timu ya taifa ya Algeria wakiwa ugenini wakipata matokeo hasi ya magoli 4 kwa 1 japo wakifanya vizuri kiasi tofauti na mechi ya mwisho ya waliyowahi kukutana na Algeria ambapo walilala kwa mabao 7 kwa 0
Walichokiomba wachezaji wa Taifa stars ni ushirikiano mzuri baina yao na bench la ufundi pia wanawaomba watanzania kuonesha uzalendo kujitokeza kwa wingi kuwashangilia kwani kufanya hivo kunawapa nguvu ya kufanya vizuri
No comments