Google AdSense

Breaking News

News : Diamond platnumz wameachana na Zari leo



Baada ya headlines za muda mrefu na mfululizo wa tetesi za penzi la Zari na muimbaji wa Bongofleva Diamond Platnumz kudaiwa kuyumba, hatimae leo Zari ameamua kuwatangazia mashabiki wake kuwa ameamua kuachana na Diamond Platnumz kwa madai ya mfululizo wa matukio ya usaliti wa kimapenzi.
Zari ametangaza kuachana na Diamond Platnumz kupitia ukurasa wake wa instagram na ameandika ujumbe mrefu ulioeleza sababu zote zilizomfanya kufikia maamuzi hayo licha ya kuwa yeye na Diamond wamezaa watoto wawili Nillan na Tiffah, kupitia ukurasa wake wa instagram Zari ameandika hivi.
“Elewa kuwa hiki ni kitu kigumu sana kwangu kukifanya, kumekuwa na tetesi mbalimbali baadhi kati ya hizo zimekuwa na ushaidi ambao umekuwa ukisambaa katika vyombo vya habari kuhusiana na usaliti wa kimapenzi unaofanywa na Diamond, kwa huzuni nimeamua kuvunja uhusiano wangu wa kimapenzi na Diamond kwa heshima yangu”
“Tunaachana kama wapenzi lakini sio kama wazazi hii hainipunguzii mimi kuwa mtu wa kujitegemea, mama mwenye kujali na Boss Lady, wote mnatakiwa kufahamu hilo nitaendelea kujijenga kama mwanamke mwenye ushawishi, nitawaamasisha wanawake wote kuwa maboss Ladies”
“Nitawafundisha watoto wangu wanne wa kiume kuwaheshimu wanawake na nitamfundisha binti yangu ni nini maana ya heshima, nimekuwa katika kiwanda cha burudani kwa miaka 12 sasa pamoja na changamoto zote hizo lakini nimefanikiwa kuwa mshindi kwa sababu mimi ni mshindi nawatakiwa wote siku njema ya wapendanao”
Kama utakuwa unakumbuka vizuri Zari na Diamond walianza kudaiwa kuwa hawapo pouwa katika mahusiano yao toka kuvuja kwa  clip video iliyokuwa inadaiwa kuwa Diamond alimpeleka msichana mwingine kulala nae Madale lakini tukio la Diamond kunaswa na camera za mapaparazi akikumbatina na mpenzi wake wa zamani Wema Sepetu wakati wa utambulisho wa  Mbosso kama msanii mpya wa WCB, kitendo kile kilidaiwa kuwa hakikumpendeza Zari.

No comments