Google AdSense

Breaking News

Ratiba ya wiki hii ligi kuu bara (VPL) hii hapa 17/18



Kuelekea mchezo mkali unaosubiriwa kwa hamu kubwa na wapenzi wa soka hasa mashabiki wa Simba pamoja na mashabiki wa Singida united, ikumbukwe kuwa mpaka sasa timu ya Singida United iliyopanda daraja msimu huu imekuwa tishio kubwa kwa timu kongwe za ligi kuu bara ikiwa na kocha mzoefu Hans Pluijm  (Yanga,Simba na Azam) na tumeshuhudia Singida united ikifanya vizuri ilipokutana na Yanga kwenye ligi kuu japo mchezo ulimalizika kwa sare tasa ya kutokufungana Lakini Singida united ndio walioonyesha kumiliki mchezo .
Baadaye Singida united walikutana na timu ya wanalambalamba Azam Fc pia walitoa changamoto kwamaana ya kutangulia kupata goli na Azam kusawazisha dakika za mwishoni kabisa ila singida walionesha mchezo wa ushindani sana kwao 
Mashabiki wa mpira wengi walitegemea Singida united wangeweza kukutana na Simba mashindano ya Mapinduzi Cup yaliyomalizika wiki iliyopita na Azam Fc wakitetea kombe Lao mbele ya URA ya Uganda Lakini timu hizi mbili Simba vs Singida united hazikukutana hapo.
Sasa imeiva mechi hiyo tunaipata kwenye mzunguko wa ligi kuu  bara siku ya kesho Alhamisi 18 Jan 18 saa 10.00 jioni nini kitatokea nani ataibuka bingwa siku hiyo, endelea kufutilia Jumbe24.blogspot.com kupata kila kinachojiri hapa Tz na Afrika  nzima

RATIBA HII HAPA

Jumatano
Yanga vs Mwadui

Alhamisi
Majimaji vs Azam
Simba SC vs Singida united

I jumaa
Mbeya city vs Lipuli Fc
Mbao Fc vs Stand united

Juma most
Tanzania prison vs Azam Fc
Mwadui Fc vs Ndanda SC

Jumapili
Ruvu shooting vs Yanga sc 

No comments