Google AdSense

Breaking News

Matokeo ya mechi zote za Mapinduzi cup 03 Jan 18 haya hapa



Michuano ya Mapinduzi Cup hatua ya makundi imeendelea jana Jumatano ya January 03-2018 kwa mechi 3 kuchezwa katika uwanja wa Amaan uliopo mjini Zanzibar.

Mchezo wa kwanza ulikuwa kati ya Mwenge dhidi ya URA timu alikwa katika mashindano hayo na URA wamefanikiwa kupata ushinidi wa goli 1-0, goli LA URA limefungwa na Bukota Lubamba katika dakika ya 27 kipindi cha kwanza, mchezo huu ulianza majira ya saa 14:30 mchana.

Ushindi huo umewafanya watoza ushuru hao wa Uganda kufikisha pointi 4, huku wakiwa wamebakiwa na mechi 2 ambazo ni Simba SC na Azam Fc.

Mechi ya pili ilizikutanisha Jamhuri dhidi ya mabingwa watetezi Azam Fc, mchezo huu ulianza majira ya saa 16:30 jioni, na Azam Fc kufanikiwa kupata ushindi mnono wa goli 4 kwa nunge.

Mabingwa hao watetezi sasa wanafikisha pointi 6 na kuongoza kundi A lenye timu za Simba, Mwenge, URA, Jamhuri, huku ikibakiza mechi 2 tu ambazo ni URA na Simba SC.

Magoli ya Azam Fc yalifungwa na Benard Arthur dakika ya 26, Salmin Hoza dakika ya 47, Yahya Zayd dakika ya 54 na Paul Peter katika dakika ya 79.

Mchezo wa mwisho ulikuwa kati Taifa Jang'ombe dhidi ya Singida United, mchezo huu ulianza majira ya saa 20:15 usiku katika uwanja wa Amaan Zanzibar.

Hadi mapumziko Singida United walikiwa mbele kwa goli 3-1, magoli ya Singida yalifungwa na Mundia dakika ya 24, Papy Kambale dakika ya 34 na Kiggi Makasi katika dakika ya 45+7.

Goli pekee la Taifa Jang'ombe lilifungwa na Meta Apingi katika dakika ya 26, baada ya timu zote kwenda mapumziko kulinyesha mvua kubwa yenye mawe katika Mji huo na kisababisha mchezo huo kuhairishwa hadi leo saa 14:30 mchana.

Dakika 45 za kipindi cha pili zitapigwa leo usiku majira ya saa 14:30 mchana, kila kitu kilichotokea katika kipindi cha kwanza kitaendelea kubaki palepale kama magoli na kadi.

No comments