Google AdSense

Breaking News

FULL MECHI KATI YA YANGA SC NA LIPULI FC

TATHIMINI YA MCHEZO KATI YA YANGA SC NA LIPULI FC



Mchezo kati ya mabingwa watetezi ligi kuu Tanzania bara Yanga SC na Lipuli FC toka mkoani Iringa umemalizika uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam kwa suluhu ya 1-1.

Lipuli ndio walioanza kutikisa nyavu za Yanga dakika ya 44 kipindi cha kwanz kwa shambulio zuri walilolijenga wing ya kulia na winga wao Seif Karie baada ya kuwazidi ujanja walinzi wa Yanga Gadiel Michael na Andrew Vincent kwa chenga safi na kupachika goli nyavuni.

Dakika mbili baadae kabla ya kipenga cha mwamuzi kupulizwa kwa ajili ya mapumziko; alikuwa ni Donald Ngoma akiruka kichwa huru na kuutia nyavuni mpira kutokana na mpira wa kona .

Timu zote zilikwenda mapumziko zikiwa suluhu ya 1-1.

JUMLA

Ni mchezo wa kwanza kwenye ligi kwa timu zote kwa msimu mpya wa 2017-18. Lipuli waliweza kuonesha uwezo mkubwa wa kuwazuia mabingwa hao wa ligi kucheka na nyavu zao. Eneo lao la ulinzi hususani walinzi wa kati , Asante Kwasi kijana toka Ghana ambaye msimu uliopita alikuwa akiichezea Mbao FC na Novalt Lufunga aliyekuwa Simba SC, waliweza kabisa kuzima mashambulizi yote ya Yanga kupitia kati kuanzia kwa kiungo wao Pappy Tshishimbi, Kamusoko , Ibrahimu Ajibu na Donald Ngoma.

Lipuli walijipanga kwa mfumo wa 4-5-1 wakijaza viungo wengi kati lakini kizuri kwao ni mfumo wa kukabia juu ambao uliwanyima fursa Yanga kutanua uwanja na kujikuta muda mwingi wakipiga pasi za nyuma au kwenye wings ambazo hazikuwa na msaada mkubwa kwao na hii ilitokana na kukosa mawinga wenye kasi kubadili mfumo wa kushambulia kutokea pembeni baada ya ' direct play ' kati kushindikana.

Emanuel Martin upande wa kushoto alishindwa kujenga mashambulizi kama ambavyo aliweza kucheza mechi ya Ngao ya hisani mechi na Simba . Muda mwingi alikuwa akifanya overlaping na Gadiel Michael ambaye kwa kiasi fulani alijaribu kupanda juu kutengeneza krosi ambazo hazikuzaa matunda. Wing ya kulia Rafael Daudi alishindwa kabisa kuisukuma timu aidha kwa kujaribu kuiyumbisha safu ya ulinzi ya Lipuli kama sprinter wa pembeni au kushambulia kwa mikwaju ya mbali kama alivyokuwa akifanya Saimoni Msuva . Ni dhahiri Rafael Daudi si msaada kwa Lwandamina kama mchezaji wa pembeni kwa mfumo wa 4-4-2 ambao kwa kiasi fulani unahitaji viungo wenye kasi pembeni. Rafael ni kiungo mzuri akichezo kati kama mchezeshaji au kiungo mshambuliaji. Muda mwingi alikuwa akizima mashambulizi kwa kukaa sana na mpira au muda mwingi kuingia kati hali iliyokuwa ikimfanya Thabani Kamusoko kutoka pembeni.

LIPULI FC

Licha ya ugeni kwenye ligi lakini kupata wachezaji wazoefu na ambao kwa kiasi fulani wanaijua vyema Yanga SC, ilikuwa msaada mkubwa kwao kutoka suluhu. Paul Ngalema akicheza kama mlinzi wa kushoto samba na Samwel Mathayo walikuwa na muunganiko mzuri na walinzi wa kati Novalt Lufunga na Asante Kwasi sambamba na mkonge Omega Seme aliyekuwa akicheza kama kiungo wa chini . Walijenga marking zone ambayo ambayo iliilazimisha Yanga kucheza mbali na eneo lao la ulinzi ( attacking zone ) . Kila Yanga walipokuwa wakijaribu kuwafanyia pressing kwa pasi fupi fupi za haraka walikuwa imara kutotoka kwenye marking zone hiyo . Walifanikiwa kwa kiasi kikubwa kuwakamata Tshishimbi na Kamusoko wasicheze huru kuwasukuma nyuma . Walipokuwa wakiona Yanga wakijaribu kuwazidi maarifa ni kuwatoa mchezoni kwa rafu au kujiangusha ili kupotez muda na kuwatoa Yanga mchezoni . Bahati mbaya mwamuzi hakuweza sana kulikemea hilo na kuwafanya Yanga kulalamika muda mwingi.

Lipuli walikuwa na marking nzuri na kiungo chao lakini bado safu yao ya ushambuliaji chini ya Malimi Busungu haikuwa vyema . Muda mwingi walikuwa wanashindwa kuipenya Ngome ya Yanga chini ya Tshishimbi, Yondani na Andrew Vicent eneo la kati. Juma Abdul kulia na Gadiel Michael kushoto ukiondoa nafasi yao moja waliyotengeneza kulia na kupata goli.

YANGA SC

Ukiondoa uwezo mdogo wa mwamuzi kulimudu pambano hususani kushindwa kung'amua mbinu za Lipuli kupoteza muda na rafu zao mbaya ; Yanga hawakuwa na mfumo mzuri kutoka na ushindi kwenye mechi hiyo.

Walicheza bila mipango ya kueleweka hususani katika mfumo wa kushambulia . Hawakuwa na kasi ya mashambulizi wala kuonesha moyo wa kujituma kutafuta matokeo kwa dakika zote 90. Walikuwa slow na kukubali kukabika kirahisi eneo la kati na kwenye wings.

Lwandamina ana kazi ya ziada kuijenga timu katika mfumo wa kushambulia kupitia pembeni . Yanga jana wameonesha endapo wakishikwa kati wanakuwa hawana tena ujanja wa kutumia viungo au mawinga wa pembeni kushambulia . Martin kushoto na Daudi kulia walishindwa kuwasukuma nyuma walinzi na viungo wa pembeni wa Lipuli baada ya muda mwingi kuonekana wakicheza kama viungo ambao wanaingia kati ilihali tayari Yanga ilikuwa imebanwa eneo hilo.

Licha ya kufunga goli zuri la kusawazisha Donald Ngoma, bado anaonesha kutokuwa sawa kwa kiwango chake cha kawaida . Ngoma mwenye nguvu , kasi ya kushambulia na kupambana na zaidi ya walinzi watatu ili kulazimisha goli. Kama angekuwa hivyo angeweza kuwaondoka Lipuli kwenye muhimili wake wa ulinzi (pivot) . Zaidi ya nafasi mbili ambazo Tshishimbi na Kamusoko walimtengenezea alishindwa kuzifata kutokana na kuonekana kukosa kasi pia clear chances mbili za kucheza na nyavu ziliishia mikononi mwa golikipa Agathon Mkwando.

Mabadiliko ya kumtoa Emanuel Martin na kuingia Yusufu Mhilu dakika ya 78 almanusura yawape goli Yanga . Lwandamina alitambua timu imebanwa kati na mawinga wake wameshindwa kusimama kama mbadala wa mashambulizi hivyo alimwingiza Yusufu kwa maelekezo ya kushambulia kwa kasi lakini nae alifanya shambulizi moja na kuingia kwenye mtego wa Lipuli wa kuwalazimisha Yanga kukaa mbali na backline yao .

Kupona kwa majeruhi Obrey Chirwa , Geofrey Mwashuiya na Amisi Tambwe inaweza kuwa msaada mkubwa kwa Lwandamina kwenye kujenga timu yenye kushambulia kwa kasi na uwezo wa kutumia kila nafasi wanayotengeneza. Kikubwa ni kutengeza wings zenye kasi na kiungo cha juu chenye muunganiko mzuri na washambuliaji. Kwa mechi ya jana ulikuwa unaona kabisa kocha anakosa mbadala sahihi kwenye benchi kuja kubadili mfumo wa kushambulia. Kidogo Ajibu alikuwa akijaribu kuwang'oa Lipuli kwenye ngome yao lakini uzoefu wa Kwasi na Lufunga ulikuwa ukiwasaidia na kujikuta muda mwingi akikaa na mpira bila malengo mazuri ya kushambulia . Inaonesha dhahiri muunganiko wake na Ngoma haukuwa mzuri . Kwa sehemu ni wachezaji wa aina moja. Wote hawakai ndani ya 18, wanacheza kama deep playmakers hivyo alihitajika mtu kama Tambwe kusimama kati na aidha mmoja wao kuanzia benchi au Ajibu kucheza saba na Ngoma kumi huku Tambwe akisimama 9. Huu unaweza kuja kuwa mfumo mzuri kwa Lwandamina dhidi ya wapinzani wake . Hii ina maana Rafael Daudi kucheza kama super sub kwenye 8,10 na 7 hususani kati au kuanza endapo kocha hatataka kumtumia Kamusoko.

Samuel Samuel

Kama ulipitwa tazama hapa mtanange wa kukata na shoka

No comments